MASHAUZI CLASSIC na JAHAZI MODERN TAARAB kuwabrudisha mashabiki wake katika show ya pamoja 22 Machi

Posted by Unknown on 02:30 with No comments
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhKBy9H3TQt8pfTI_ona4eo3g1EfrOuiWSEao61NOGe0F_pPIr8PghyphenhyphensIWcprQjyW5r1MG8iowbKAxLzjx0TyA-BRr9y_4BHPEKulDZGDidqZK0Bj4T-U1siHsSciO64PYzbEfCnxBtvFQ/s1600/unnamed+(28).jpg

 Hayawi hayawi sasa yamekuwa.......Yale makundi makubwa ya muziki wa mwambao alimaarufu kama Taarabu  MASHAUZI CLASSIC na JAHAZI MODERN TAARAB wameamua kukutana na kufanya show ya pamoja ili kukonga zaidi nyoyo za mashabiki wake kwa kuwapa radha moja matata kwa mpigo.
Makundi haya yanayoaminika kuwa ndio yenye mashabiki wengi sana kwa upande wa taarabu yamepanga kutoa show hyo ya pamoja itayofanyika Travertine Hotel iliyopo MAGOMENI  ndani ya jiji la Dar es Salaam tarehe 22 mwezi March siku ya Jumapili.

Onyesho hilo limelenga kukuza udugu pamoja na kuwakutanisha pamoja mashsbiki wao na siyo kupambanisha yupi ni bora zaidi. Tamasha kama hili limewahi kufanyika katika hotel ya TRAVERTINE miaka takribani minne iliyopita na rekodi ya mahudhurio haijavunjwa hadi leo.......NI USIKU WA BABA NA MWANA  Part 2.........Dont miss uhondo!!!!!!!!!!!!!!!!!



Categories: ,